.

5/27/2021

Makasiriko, Harmonize Aifuata Collabo kwa Madiba

 


Mwanamuziki na Boss wa Konde Music Worldwide yupo kwa Madiba na amefanikiwa kuingia studio kutengeneza wimbo na nyota wa muziki Busiswa Gqulu ambaye ndiye mwenyeji wake huko nchini Afrika Kusini. 

 

Harmonize ambaye yupo mbioni kuachia album yake mpya, 'High School' ame-share vipande vya video na taarifa ya collabo hiyo kupitia insta story yake.


Mwanadada Busiswa ni mwimbaji kutoka Afrika Kusini, ambaye amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Beyonce kupitia mradi wa "The Lion King, The Gift" ambapo alisikika kupitia wimbo uitwao 'The Power' pia ni mshindi wa Tuzo mbalimbali kubwa za muziki ikiwa ni pamoja na za Channel O Afrika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger