.

5/30/2021

Mo Dewji Ampa Shavu Mondi
Mfanyabiashara na bilionea maarufu Bongo, Mohamed Dewji amempongeza Msanii machachari wa Bongofleva, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’ kwa kuteuliwa kuwania tuzo za BET awards.

 

Mo ambaye ni Mwekezaji na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba, kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika, hongera sana @DiamondPlatnumz kwa kuteuliwa kuwania tuzo za #BETawards katika kipengele cha ‘Best International Act’. Tunajivunia uwepo wapo katika kukuza Bongofleva duniani.

 

Katika tuzo hizo Diamond anachuana na Wizkid, Burna Boy, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey.

 

Hii ni mara ya tatu Diamond Platnumz kuchanguliwa kuwania tuzo za BET ambazo zinafanyika Juni 28, 2021. Mwaka 2014 alitajwa kwa mara ya kwanza kuwania tuzo hizo na mara ya pili ilikuwa mwaka 2016.

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger