Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mondi Aishi Kama Kifalme Afrika Kusini

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa sasa anaishi maisha ya kifalme nchini Afrika Kusini (Sauzi).

 

Hivi karibuni, Diamond au Mondi alikwea pipa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi wakati huu akiandaa albam yake mpya atakayoiachia baadaye mwaka huu.

 

Tangu ajichimbie nchini humo ambako pia kuna watoto wake wawili aliozaa na mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tiffah Dangote na Prince Nillan, wengi walidhani angeenda kuishi nyumbani kwa mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo lilizua minong’ono kwamba huwenda wakarudiana.

 

Hata hivyo, habari za uhakika ni kwamba, Mondi anaishi kwenye apartment yeye pamoja na timu, lakini akitaka kuwaona watoto wake amekuwa akiwafuata kwa Zari au kuletewa anapoishi.Sababu ya kwa nini ameamua kuishi kwenye apartment ilihali ana familia nchini humo haijawekwa bayana.

Uamuzi huo wa Mondi unatajwa kuwa tofauti na ule wa Zari ambaye alipotinga Bongo mwishoni mwa mwaka jana, alilala nyumbani kwa Mondi, Mbezi-Beach jijini Dar.

Vyanzo vya ndani vinadai kwamba, Mondi ameamua kuishi kwenye apartment kama sehemu ya kupata utulivu na kuwa huru kwa ajili ya kuandaa albam yake hiyo itakayoweka historia barani Afrika.Hata hivyo, gumzo kubwa ni juu ya mjengo anaoishi wa kifahari na namna ulivyowekewa ulinzi mkali kwa kuwa nchi hiyo inadaiwa kuwa na magenge ya wahalifu hivyo amekuwa akiambatana na mabodigadi kila anakokwenda.

 

Kwenye mjengo huo anaoishi wa kifahari una kila kitu kinachopatikana kwenye makasri ya kifalme kama mabwawa ya kuogelea, gym, studio, ukumbi wa kuangalia sinema na vingine vingi.Mondi amekuwa akiachia video mbalimbali kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii zikimuonesha akiwa kwenye mjengo huo akiendelea na shughuli zake za kimuziki.Katika moja ya video hizo aliandika; “Nyumbani kwangu kupya kwa muda wa mwezi mmoja…kumalizia albam yangu.


Post a Comment

0 Comments