.

5/24/2021

RC Makalla akutana na Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo May 24 ameanza rasrmi majukumu yake kwa kukutana na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam ambapo ameweka utaratibu wa kufanya kikao nao kila baada ya miezi mitatu.


RC Makalla amesema anatambua thamani na Mchango wa Wazee Katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na Baraka zao kwani anatambua Wazee ni hazina Muhimu.

Aidha RC Makalla amesema Katika kutatua kero na changamoto za Wananchi amepanga kuanza ziara ya utatuzi Kata kwa Kata hivyo amewahakikishia wananchi kuwa anayo dhamira ya dhati kuzipatia majibu kero zao.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwakuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Mkoa mkubwa na Wenye kutoa taswira ya nchi nzima kwenye kila nyanja mbalimbali, amejipanga kuhakikisha Jiji linakuwa shwari na watu wanafanya shughuli zao pasipo usumbufu wowote Kama maono na mategemeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wao Wazee walioshiriki kikao hicho kwanza Wamemshukuru na Kumpongeza RC Makalla kwa namna anavyoheshimu Wazee na wamemuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha Katika majukumu yake. Aidha Wazee hao wamesema Wana Imani kubwa na RC Makalla kwakuwa wasifu wake wa uongozi unaonyesha kila alipopita amekuwa akiacha alama hivyo wanaamini atafanya Mambo makubwa na Mazuri Katika Mkoa wa Dar es salaam

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger