Shambulio la ndege za Israeli lawauwa watoto katika kambi ya wakimbizi

Takriban watu 13 wameuawa, waliwemo watoto wanane, katika amshambulio ya anga yaliyopiga kwenye kambi ya wakimbizi ya Gaza.


Muhammad Hadidi, baba ambaye watoto wanne wameuawa katika shambulio hilo lililopiga kwenye kambi ya wakimbizi ya Shati iliyopi mjini Gaza, anasema amepoteza kila kitu.Mke wake , Maha, na watoto walikuwa wakiishi na kaka yake wakati jingo lilipowaangukia.Mtoto wake mchanga wa miezi mitano Omar, anasemekana kuwa ndiye pekee aliyenusurika, baada ya kupatikana akiwa amekwama kwenye vifusi vya jingo lililopigwa na ndege za Israeli , akiwa kando ya mama yake ambaye amekufa.Hadidi anataka "dunia isiyo na haki kuona uhalifu huu", aliliambia shirika la habari la AFP , alipokuwa akizungumza nalo nje ya hospitali ya Shifa mjini Gaza."Walikuwa salama katika nyumba zao , hawakuwa wamebeba silaha, hawakuwa wamebeba maroketi," alisema kuwahusu watoto wake ambao "wakiwa wamevaa nguo zao walizonunuliwa kwa ajili ya Eid al-Fitr".Kwa ujumla, mashambulio ya anga yamewauwa watu 10 kutoka katika ukoo mmoja, wakiwemo watoto wanane, kwa mujibu wa maafisa wa Palestina mjini Gaza.Wakati huo huo jengo lenye ofisi za vyombo vya habari lilianguka baada ya mashambulio ya ndege za IsraeliJengo la gorofa mjini Gaza, lenye ofisi za vyombo vya habari Associated Press (AP) na Al Jazeera limeanguka baada ya kupigwa na shambulio la kombora la ndege ya Israeli.Wafanyakazi walikua tayari wameondoka kwenye jengo hilo baada ya mmiliki wake kupata onyo kutoka kwa Israeli mapema juu ya mashambulizi, linasema Shirika la habari la Reuters.Mapema madaktari wa Israeli walisema kuwa mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 na zaidi aliuawa wakati jengo moja lilipopigwa na roketi katika kitongoji cha mji mkuu wa Israeli Tel Aviv cha Ramat Gan.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE