Ukaguzi wa nyimbo wapigwa 'STOP'

 


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, amesema kuwa serikali imesitisha utekelezaji wa kanuni za kukagua nyimbo za wasanii kabla hazijapelekwa kwenye Radio, Televisheni na majukwaa mbalimbali.


Uamuzi huo umetolewa leo Mei 8, 2021, mara baada ya waziri mwenye dhamana hiyo kukutana na wadau wa muziki nchini wakiwemo wasanii wenyewe.


Waziri Bashungwa amechukua uamuzi huo baada ya wadau wa muziki kupinga suala hilo wakidai haliwatendei haki wasanii.


Hatua hii inakuja zikiwa zimepita siku kadhaa tu tangu BASATA walipouzia wimbo wa msanii Ney wa Mitego, kwa kumtaka abadili baadhi ya mashairi kwenye wimbo wake wa Mama, ambapo Ney mwenyewe alisema kwamba hayuko tayari kubadili chochote kwenye wimbo wake

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE