.

6/05/2021

Azam Kukupiga na Coastal Union Leo
Wanalamba lamba, klabu ya Azam inataraji kucheza mchezo wa kirafiki saa 1:00 usiku wa leo Juni 6, 2021 dhidi ya Wagosi wakaya, klabu ya Coastal Union kwenye dimba la Chamazi, Temeke jijini Dar es Salaam.

 

Mchezo huo unataraji kuwa kupasha misuli kwa timu zote mbili ambazo zinashiriki ligi kuu soka Tanzania bara, Azam ikishika nafasi ya tatu wakiwa na alama 60 baada ya kucheza michezo 30, utofauri wa alama 7 na wakiwa mbele kwa michezo 3 mbele ya kinara Simba Sports Club.

 

Wagosi wakaya wapo nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 29 na kujizolea alama 33 ambazo zinawafanya wawe kwenye hatari ya kushuka daraja endapo wakimaliza kwenye nafasi hiyo huku wakihaha kumaliza kwenye nafasi ya 12 ambayo inashikiliwa na Ihefu yenye alama 32.

 

Mchezo huo unachezwa kwenye dimba hilo baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na African Lyon wa daraja la kwanza uliopangwa uchezwe saa 1:00 usiku wa leo kughahirishwa na klabu ya Yanga ambao hawakuweka wazi sababu za kughairisha mchezo huo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger