.

6/03/2021

Kutana na Jamaa Aliyewahi Kumshitaki MUNGU MahakamaniJAMAA ALIYEWAHI KUMSHTAKI MUNGU MAHAKAMANI BADO ANAISHI ; Seneta Ernie Chambers wa jimbo la Nebraska, Marekani mwaka 2008 alimshitaki Mungu akiiomba Mahakama itoe zuio la kudumu dhidi ya Mungu kufanya shughuli zake zenye madhara kama mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, tufani na majanga mengine

Inadaiwa katika shauri hilo watu wengi wamekuwa wakijitambulisha kama Mawakala wa Mungu na kufanya mambo mengi maovu lakini hata siku moja Mungu hajajitokeza hadharani kuwakana hivyo wanafanya yote kwa niaba yake na jina lake

Mahakama ilimtaka Seneta Chambers kuhakikisha anamtaarifu Mungu kuhusu uwepo wa shauri hilo dhidi yake Mahakamani hapo kwa kumtumia nyaraka zote za kesi kupitia anuani rasmi ya Mungu ili aweze kufika Mahakamani hapo kujibu madai dhidi yake

Seneta Chambers aliiambia Mahakama kuwa Mungu yupo kila mahali na anajua kila kitu. Hivyo anajua kuhusu uwepo wa shauri dhidi yake Mahakamani hapo wala hakuna haja ya kumtaarifu labda aamue mwenyewe kutokuja kama ilivyo kwa wadaiwa wengine

Julai 10 mwaka huu bwana huyu atatimiza umri wa miaka 84 🎂
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger