Mbunge Atoa MPYA..Apendekeza Bodaboda Wafungiwe Leseni zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira, ametoa pendekezo kwa serikali kuhusu faini ya bodaboda na bajaji kwamba waweke mifumo kwenye leseni za madereva hao utakaoruhusu dereva kulipa faini kwa makosa mawili pekee na akitenda kosa la tatu basi afungiwe leseni yake. um Neema Lugangira


Kauli hiyo ameitoa leo Juni 23, 2021, wakati akitoa mchango wake katika muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2021, na kuongeza kuwa serikali isiache faini ya shilingi 10,000 pekee kwa bodaboda ama madereva bajaji bali iweke na mfumo wa kuwawajibisha huku lengo likiwa ni kulinda maisha ya watumiaji wa usafiri huo pamoja na bodaboda wenyewe.

"Kuhusu faini za bodaboda ningependa kupendekeza kwa serikali ije na mfumo wa kuweka 'point system' kwenye hizi leseni kwamba huyu mwendesha bodaboda au bajaji akifanya kosa la kwanza na la pili alipe 10,000, akifanya kosa la tatu kulingana na ile point system leseni yake ifungiwe kwa kufanya hivyo tutalinda watumiaji wa zile pikipiki na maisha yao wenyewe tusiache hii faini ya elfu 10 pekee yake,"amesema Mhe. Neema Lugangira

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad