Tanzania Yaendelea Kushika Nafasi Ya 10 Bora Kwenye Utalii Bara La Afrika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





NA MWANDISHI WETU, WINDHOEK, NAMIBIA.
TANZANIA imeendelea kung'ara ndani ya Bara la Afrika kwa kutangaza vyema vivutio vyake vya Utalii ambapo imeweza kuwa miongoni mwa nchi  10 bora kwa mwaka wa tatu mfululizo, kuanzia 2017 hadi  2020.

Ripoti hiyo imetolewa mapema leo  kwenye mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Utalii  Duniani  (UNWTO), Mtaalamu wa utangazaji wa Utalii, Bi. Olga Nowak aliitangaza Tanzania kushika nafasi ya saba  ambayo inakuwa ni mara ya tatu.

Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Watalaamu wake kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wanashiriki  ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania

Katika kumi bora hiyo,   Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza  ikifutiwa na nchi ya  Misri  katika utangazaji vyema  ya vivutio vyake vya  utalii.

Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa  kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19  ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.

Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro

Katika hatua nyingine  Tanzania kushiriki katika mkutano huo kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu  imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo

Pia, Tanzania imepata  fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad