Tanzia: Mwigizaji wa Mizengwe Maarufu Mzee Matata Afariki Dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


MWIGIZAJI wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela almaarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, 2021.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo Jumatano Juni 16, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Juni 13, 2021.

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, @madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar es salaam.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa

“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” taarifa kutoka kwa @madebelidai.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad