Uongozi wa Simba watangaza kuachana na Ajibu, Gadiel Michael

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






RASMI uongozi wa Simba umetangaza kuachana na wachezaji wake wawili kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu na beki wa kushoto Gadiel Michael.
Simba inaachana na wachezaji hao kama wachezaji huru kutokana na mikataba yao kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Awali tetesi zilizagaa za wachezaji hao kuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Yanga katika kuelekea msimu ujao kabla ya mashabiki kuja juu kushinikiza viongozi kusitisha mipango hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, timu hiyo haipo tena katika mipango ya kuwaongezea mikataba mipya ya kuendelea kuichezea timu hiyo, ni baada ya Benchi la Ufundi kupendekeza kuachana na nyota hao.

Chanzo hicho kilisema kuwa Simba inamsaka mbadala wa Gadiel ambapo awali ilikuwa inamhitaji Edward anyama kabla ya mabosi wa Azam FC kupindua meza kibabe.

Kiliongeza kuwa mabosi hao hivi sasa wapo katika mipango ya kumpata kiungo mwingine mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao atakayemrithi Ajibu.

“Rasmi Gadiel na Ajibu ruksa hivi sasa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayowahitaji katika kuelekea msimu ujao, kwani hawapo katika mipango yetu.

"Hivi sasa ni wachezaji huru kwani mikataba yao tayari imemalizika, kwani wale wachezaji wetu wote muhimu waliokuwepo kwenye mipango ya kocha tumewaongezea mikataba mipya," ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumzia usajili wa timu hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alisema: “Muda wa usajili bado, lakini pia mipango yote ya usajili ipo kwa kocha wetu Gomes (Didier) ambaye ndiye atakayependekeza wachezaji wa kusajiliwa na kuachwa.”

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad