.

7/23/2021

Hoteli Yaungua Kariakoo, Wawili Wakimbizwa Muhimbili
Vikosi vya uokoaji na usalama vikiwa kazini.
Hoteli maarufu ya Kibo Palace iliyopo Kariakoo Jijini Dar, leo majira ya kuanzia saa tano asubuhi ilianza kuungua moto ambapo mpaka muda huu bado vyombo za ulinzi la usalama vinaendelea na jukumu la usalama wa eneo hilo. Global Publishers ilifika eneo la tukio na kukuta  juhudi za uokoaji zikiendelea ambapo Mrakimu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto Mkoa za Zimamoto wa Ilala, Elisa Kamugisha amesema moto huo ulianzia gorofa ya tano.


Muonekano wa hoteli hiyo baada ya jitihada za Jeshi la Zimamoto kuzima moto huo.
“Huu moto ulianzia gorofa ya tano ambayo wamekuwa wakiitumia kama stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali ambapo baada ya moto kuanza na kuwazidi nguvu walitupigia simu na tunashukuru tumefika kwa wakati.

“Licha ya moto huo kupamba katika gorofa ya tano jengo zima lilitawaliwa na moshi na kuwafanya waliokuwemo kushikwa na taharuki lakini kwakuwa tuliwahi ikabidi askari wetu wa uokoaji watumie mafunzo kwenda kuwaokoa.

Mpaka hivi tunavyoiongea ni watu wawili akiwemo raia wa Senegal ambao wameumia katika harakati za kutaka kujiokoa na wameshakimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu” alisema Kamanda Mugisha.  HABARI/PICHA RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger