.

7/24/2021

Kanye West Ashirikiana na Hasimu Wake Jay-Z

RAPA Kanye West amefichua kwamba Jay-Z ni miongoni mwa wasanii walioshiriki katika albamu yake mpya alioizindua. West aliandaa sherehe ya albamu hiyo ya Donda aliyoipatia jina la mamake ambaye ni marehemu katika uwanja uliofurika wa Mercedes Benz, mjini Atlanta katika jimbo la Georgia, mji aliozaliwa.

 

Akivalia jaketi la rangi nyekundu , lililofanana na suruali aliyovaa na viatu vya rangi ya machungwa zote zikiwa na nembo yake, Yeezy Mogul,44 , usoni alivalia kile kilichoonekana kuwa barakoa iliotengenezwa na mpira.

 

Aliingia katika ukumbi bila kusema na albamu ikaanza kuchezwa bila utangulizi rasmi kutoka kwa mtengenezaji wake. Wimbo wa mwisho ulimshirikisha Jay-Z, rafiki yake wa siku nyingi , mpinzani na mshirika wake. Mshororo mmoja wa Jay-Z ulishirikisha neno ‘’red cap’’ akimaanisha kofia ya Kanye West ilioandikwa MAGA {‘Make America Great Again’}.

 

Young Guru, mzalishaji wa muziki na muhandisi ambaye amefanya kazi na Jay-Z, alifichua kwamba mshororo huo uliongezwa dakika za mwisho , pengine akielezea kwanini sherehe hiyo ilichelewa kwa saa mbili. Alituma ujumbe wa twitter: ‘’HOV aliimba mshororo huo hii leo!!! Saa 10 jioni’’.

 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger