Kimanza Kunuka Kigoma... Yanga Waomba Mwamuzi AbadilishweUongozi wa Klabu ya Yanga Sports Club, umesema umeshtushwa na na chaguo la Mwamuzi Ahmed Arajiga kuchezesha mchezo wa Fainali za Kombe la Shirikisho (ASFC) utakaochezwa Kigoma Jumapili hii Julai 25.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na idara ya habari ya klabu hiyo, hali hiyo imetokana na kuwa mwamuzi huyo amechezesha mechi zilizofuatana za wapinzani wao Simba katika mashindano hayo katika hatua ya Robo Fainali, Nusu na sasa Fainali.

Taarifa hiyo imeeleza, kitendo cha kumrudia mwamuzi huyo katika mechi tatu za timu moja na shindano moja, kimewatia mashaka hivyo wanaomba TFF watafakari juu uamuzi wa kumtumia mwamuzi huyo.đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad