.

7/17/2021

Mapya yafichuka tukio la mpenzi aliyechomwa ndani ya nyumba
Wakati Jeshi la Polisi Kanda Maalum likimshikilia Grace Mushi (25) kwa tuhuma za kumchoma moto ndani ya nyumba aliyekuwa mpenzi wake, Khamis Abdallaah (25), mashuhuda wa tukio hilo wamefichua mambo mazito.


Mapema leo Jumamosi Julai 17, 2021 Kamanda wa Kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Julai 16 saa nane usiku maeneo ya kwa Mzungu Mbezi Makabe wilayani Ubungo.Amesema mtuhumiwa aliamka usiku na kumfungia ndani Khamis kisha kumwaga petroli na kuichoma moto nyumba hiyo kitendo kilichosababisha kifo cha mwanaume huyo.Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na Mwananchi, wamesema kuwa Khamis alikatazwa kuwa na mahusiano na mtuhumiwa.Mmoja wa mashuhuda hao Ramadhan Ondolo, ambaye ni rafiki wa Khamis maarufu kama Zungu, amesema kuwa aliwahi kumsihi rafiki yake kutokuwa na mahusiano na mwanamke huyo.Amesema siku ya tukio mchana alionana na Zungu akamuomba azungumze naye, lakini akamwambia kuwa atamtafuta baadaye.“Kabla ya tukio ilikuwa mchana majira ya saa nane, alinipigia simu akaniambia kuna hela zangu anataka anipe, nikamwambia sawa haina shida, akazunguuka akarudi akanipa, sasa mimi nilitaka kuongea naye kuhusu huyu msichana ila akataka tuzungumze baadae  basi nikamuacha.“Niliwahi kumkataza na hata hayo maongezi yetu yalikuwa ni hayo, nilitaka nimkataze aache kuwa na mahusiano na Grace kwa sababu hawaendani. Mara kadhaa nimemkataza nikimtaka apambane familia yake. Kila ninapokuwa naye namwambia hivyo,” amesema.“Usiku kama kwenye saa nane nikapigiwa simu na mtu ambaye anafanya naye kazi hapo saluni, nikajiuliza huyu saa hizi anataka nini nikaacha sijapokea nikaja nikapigiwa na mtu mwingine jirani ndio akaniambia rafiki yako amepata ajali ya moto. Awali, nikajua labda pikipiki imelipuka na sikufikiria kama itakuwa ajali ya namna hiyo. “Usiku huo huo nikatoka nyumbani na mke wangu kufika nikaambiwa Zungu yupo ndani anaungua hivyo, tukaanza kufanya juhudi za kumuokoa lakini ikashindikana,” ameongeza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. Thank you quite much for discussing this type of helpful informative article.
    Will certainly stored and reevaluate your Website.

    Feel free to visit my page :: 강남오피
    (jk)

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger