Rais Samia Aguswa na Malalamiko ya Tozo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais Samia Suluhu Hassan ameguswa na malalamiko ya wananchi kuhusu tozo za miamala ya simu iliyoanza kutumika hivi karibuni na kuwaagiza mawaziri husika kutafuta suluhisho.


Hayo yamesemwa leo Julai 19 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kupitia televisheni ya Channel Ten, akisema pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa na kikao na mawaziri husika ili kutafuta suluhisho.


“Tayari Mheshimiwa Rais ameshaguswa na jambo hili amesikia maoni ya Watanzania wote na amesema tuyafanyie kazi jambo hili,” amesema Waziri


Dk Mwigulu ameongeza kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na Waziri Mkuu. “Vilevile Waziri Mkuu ameitisha kikao kitakachofanyika kesho (Julai 20) kuendelea kupitia jambo hilo hilo.”


Amesema Serikali imesikia kilio cha wananchi na kuna mambo watakayoyafanyia kazi na mengine wataendelea kuwaelimisha wananchi.  


“Tumepokea maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa uelewa zaidi kwa maana ya uelimishaji zaidi ili kuwa na uelewa wa pamoja, ikiwa pamoja na viwango vinavyokatwa, yupi anayekatwa, ukataji wakati wa kutoa na mantiki ya jambo hili zima kwa ujumla,” amesema


Source: Mwananchi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad