Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Sarpong Mambo Safi Yanga, Metacha Ajadiliwa
UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umeweka wazi kuwa tayari umemalizana na mchezaji Michael Sarpong, kuhusiana na matatizo ya kinidhamu, na sasa ni Metacha Mnata pekee ambaye suala lake linajadiliwa na Kamati ya Nidhamu.

 

Metacha amesimamishwa na klabu hiyo kwa utovu wa nidhamu aliouonesha mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Juni 17, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Wachezaji ambao walikuwa na matatizo ya kinidhamu wengi wao tayari changamoto zao zilishamalizwa, kuhusu Sarpong ishu yake ilimalizika na tayari amejiunga na kikosi licha ya kwamba alipata majeraha.

 

“Mchezaji pekee ambaye suala lake linaendelea kujadiliwa ni Metacha Mnata, ingawa tayari alishaadhibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), taarifa yake itatolewa hivi karibuni.”


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments