Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Simulizi ya Mgonjwa wa Corona

 


Mwanadada Neema mkazi wa Dar es Salaam, ametoa simulizi yake namna alivyoanza kuumwa kifua, mafua na mwili kuishiwa nguvu katika wimbi hili la tatu la maambukizi ya Virusi vya Corona hadi baadaye alipokuja kugundulika na ugonjwa huo.

Akizungumza huku akitoa sauti kwa shida kidogo hii leo Julai 12, 2021, kupitia kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, Neema amesema kuwa dalili za awali alizozipata alihisi pengine ni mzio (Allergy) ama vumbi na akaanza kunywa chai yenye limao ndani yake.

"Baadaye nikaanza kutumia dawa kwa ajili ya kifua, nikaamua kwenda hospitali nikafanyiwa vipimo na muda huo mwili ukaanza kuchoka, nikapimwa kila kitu nikaambiwa nina UTI na nikapewa antibiotic lakini baada ya kurudi nyumbani nikawa napata homa kali," amesimulia Neema

Sehemu ya pili ya simulizi hii ya Neema itaendelea kesho kwenye kipindi cha SupaBreakfast kinachoanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments