.

8/21/2021

Askofu Gwajima na Silaa kufika mbele ya Kamati

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ameamuru Mbunge Josephat Gwajima na Mhe. Jerry Silaa kupelekwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya bunge.


Kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge Leo jijini Dodoma imeeleza kuwa Mhe. Gwajima anatakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo siku ya jumatatu tarehe  23, Agosti 2021 saa saba mchana huku Mhe. Silaa akitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo tarehe 24/08/2021 saa saba kamili mchana katika ofisi za Bunge.Kwa mujibu wa kanuni 4(1) (a) na (b) ya nyongeza ya nane ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Juni 2020 ambayo inaipa mamlaka Kamati hiyo kuchunguza mambo yanayohusu maadili yanayopelekwa na spika, hivyo basi wabunge hao wanatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo.Aidha endapo waheshimiwa hao hawatafika mbele ya kamati kwa siku na muda uliotajwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger