.

8/08/2021

Brazil yanyakua medali ya dhahabu Olimpiki

BRAZIL imefanikiwa kutwaa Medali ya Dhahabu kwa mara ya pili mfululizo kwenye Michezo ya Olimpiki upande wa soka baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Hispania ndani ya dakika 120 Uwanja wa Nissan Jijini Yokohama,.

Dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 Matheus Cunha akiitanguliza Brazil dakika ya 45 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Dani Alves, kabla ya Mikel Oyarzabal kuisawazishia Hispania dakika ya 61 kwa usaidizi wa Carlos Soler – na Malcom akafunga la ushindi dakika ya 108 kwa pasi ya Antony.

Wakati Brazil ikibeba Medali ya Dhahabu, Hispania wamechukua Fedha na Mexico iliyomaliza nafasi ya tatu baada ya kuwafunga wenyeji, Japan 3-1 jana wameondoka na Shaba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger