.

8/24/2021

Jerry Silaa aingia na lundo la vitabu, agoma kusindikizwa na askari 
Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ameingia kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku akiwa na lundo la vitabu mbalimbali  11 ikiwamo biblia.

Silaa ameingia kuhojiwa saa 8:43 mchana ndani ya ukumbi wa kamati inayoongozwa na Mwenyekiti wake Emmanuel Mwakasaka ambapo baada ya kuingia ukumbini alipuliza kitakasa mikono kwenye kipaza sauti(MIC) na kufungua begi kubwa lililokuwa limejaa vitabu hivyo.

Awali, wakati akiingia katika viwanja vya bunge amekataa kusindikizwa na askari kama ilivyokuwa kwa Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima.

Hata hivyo, baada ya mabishano Silaa alikubali kuongozana na askari hao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger