.

8/24/2021

Miili ya Watumishi Watano TRA Yaagwa
Vilio na majonzi vimetawala hii leo Agosti 24, 2021, katika viwanja vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Mbeya, wakati wa kuaga miili ya wafanyakazi watano wa TRA kikosi kazi cha fast track waliofariki dunia hapo jana kwa ajali ya gari mkoani Songwe.

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Hanseketwa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe majira ya saa 11 alfajiri jana Agosti 23, 2021 baada ya gari lao aina ya Landcruiser yenye nambari za Usajili STL 8825 Mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambalo liligonga Lori aina ya FUSO yenye nambari za usajili T 586 ANE.

Watumishi wa TRA waliofariki ajalini ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi. Miili yao itasafirishwa kwenda mikoa mbalimbali ambako kila mmoja ni nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger