.

8/04/2021

Mume amuua mkewe kwa kumkata na panga kisa wivu wa mapenzi
Mkazi wa kata ya Malezi wilayani Handeni mkoani Tanga, Nassoro Mustapha anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali mwilini ikielezwa sababu ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea jana Agosti 3, 2021 katika mtaa wa Kwamaraho iidaiwa kuwa mwanaume huyo alikuwa na ugomvi na mkewe na ndio uliomrudisha nyumbani.

Dada wa marehemu, Rehema Hemed amesema wanahisi tukio hilo limetokana na wivu wa mapenzi kwa sababu wanandoa hao walikuwa na ugomvi na kwamba shemeji yake alikuja nyumba wakiwa hawapo na kumshambulia mdogo wake.

"Nilikuwa kazini nikapata taarifa kwamba mdogo wangu amekatwa panga na mumewe, tulifika nyumbani na kumkuta amejeruhiwa mwili lakini alifariki tukiwa njiani kumpeleka hospitali, "amesema Rehema.

Rehema amesema ndugu yake amefariki akiwa ni ujauzito wa miezi sita au na ameacha mtoto wa miaka mitatu.

Diwani wa Malezi, Shabani Kitombo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ni la pili katika mtaa huo mwaka huu.

"Nilivyoelezwa huyu binti amechalazwa mapanga maeneo ya shingoni na mumewe na chanzo cha ugomvi ndugu zake wanahisi ni sababu za mapenzi na mhusika anaendelea kutafutwa baada kukimbia, " amesema Kitombo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger