.

8/03/2021

Mwanaume huko Senegal avalia kama msichana kumfanyia mpenzi wake mtihani
Mwanafunzi wa chuo kikuu huko Senegal yuko amejipata mashakani baada ya kuvalia kama mwanamke ili kumfanyia mpenzi wake mtihani wa somo la Kiingereza.

Picha za Khadim Mboup akiwa amevalia nguo za wanawake zimesambazwakatika mitandao ya kijamii na katika vyombo vya habari nchiniSenegal.

Mwanafunzi huyo wa miaka 22, ambaye alikamatwa mwishoni mwa wiki, alisema alikuwa akifanya hivyo kwa "kwa sababu ya mapenzi " kwa sababu mpenzi wake alikuwa na shida katika somo la Kiingereza, vyombo vya habari vya huko viliripoti.

Alifikishwa mbele ya korti Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa utambulisho na udanganyifu wa mitihani pamoja na mpenzi wake , ambaye alishtakiwa kuhusika katika uhalifu huo.Pulse Sénégal iliweka picha hiyo kwenye Twitter:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger