Ndugu wa Hamza wangewajibika tusingekuwa hapa- IGP



 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka wazazi kuhakiksha wanashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama pale wanapokuwa na watoto majambazi ama magaidi na wale wenye tabia za hovyo hovyo ili kuweza kuepusha madhara kwenye jamii.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro,
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 27, 2021, wakati wa kuaga miili ya Askari akiwemo mmoja kutoka kampuni ya ulinzi binafsi ya SGA, waliofariki dunia baada ya kushambuliwa kwa risasi na mtu aliyeleta taharuki maeneo ya daraja la Selander karibu na zilipo ofisi za Ubalozi wa Ufaransa mnamo Agosti 25 mwaka huu.

"Huyu Hamza aliyoyafanya kama ndugu zake wangewajibika vizuri leo tusingekuwa hapa, lakini watanzania wenzangu waelewe siku zote Askari Polisi na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili ya kulinda watanzania na ndiyo maana tumeapa kufa kwa risasi, lakini lazima mjue na sisi tuna familia zetu," amesema IGP Sirro

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad