.

8/25/2021

Njaa Madagascar yawalazimisha watu kula wadudu
Madagascar iko katika ukingo wa kukumbwa na ''njaa inasobabishwai na mabadiliko ya hali ya hewa", kulingana na Umoja wa Mataifa ambayo inasema maelfu ya watu tayari wanakabiliwa na viwango vya juu vya njaa na uhaba wa chakula baada ya kukosa mvua kwa miaka minne.
Ukame huo - mbaya zadi kuwahi kushuhudiwa ndani ya miongo minne - umeathiri zaidi jamii ya wakulima kusini mwa nchi, na kuwa fanya wageukie kula wadudu ili kuishi.

"Hii ni hali ya njaa inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa sio mizozo," alisema afisa wa Shirikala Chakula la Umoja wa Mataifa, Shelley Thakral.

UN inakadiria kuwa watu 30,000 kwa sasa wanabiliwa viwango vya juu vya uhaba wa chakula uliotambuliwa kimataifa - na kuna wasi wasi kwamba idadi ya walioathirika ikaongezeka pakubwa wakati Madagascar inaingia ''msimu mwembamba'' kabla ya mavuno.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger