Rais wa zamani wa mpito wa Mali aondolewa katika kizuizi cha nyumbani





Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi - ECOWAS imesema rais wa zamani wa mpito wa Mali, Bah Ndaw na waziri mkuu wake Moctar Ouane wameondolea katika kizuizi cha nyumbani.
 
Katika taarifa hiyo ya ECOWAS inaikaribisha hatua hiyo ya Mali, ya kuowaondolea vizuizi viongozi wote wa zamani na kusema viongozi wote hao wawili wanapaswa kupata fursa na haki zote za kimsingi kama rais wa zamani na waziri mkuu wa zamani.
 
Kabla ya kuondolewa madarakani katika mapinduzi ya pili na Kanali Assimi Goita, rais huyo wa zamani wa mpito wa Mali, Bah Ndaw na waziri mkuu wake Moctar Ouane walichaguliwa kama viongozi wa kiraia baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 2020.
 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad