Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Ajali ya Coaster Yaua 6 Mbinga
BAD NEWS: Watu sita wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Septemba 17, 2021 katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wakati wakisafiri kwa basi aina ya Coaster kutoka Dar es Salaam kuelekea Nyasa kwa shughuli za kifamilia.
Basi hilo lililokodiwa lilipinduka katika mlima Kipololo uliopo wilayani Mbinga wakati likiwa njiani kuelekea Lundo, Nyasa.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na vifo vya watu sita na ameahidi kutoa taarifa zaidi za tukio hilo leo asubuhi.
 
Kwa upande wake, Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Mbinga, Dk Shila Mishiuya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri miili pamoja na majeruhi wa ajali hiyo.
 
Amesema idadi kamili ya majeruhi bado haijajulikana na kwamba atatoa taarifa kesho baada ya kupokea miili na majeruhi wa ajali hiyo.

OP

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments