.

9/07/2021

Askofu Gwajima Aungana na Rais Samia..“Wiki hii Rais Samia wakati anaenda Bagamoyo akapita Tegeta kwenye Jimbo la Kawe, kuna jambo lilinigusa sana alipokuwa anaongea akasema ameamua atengeneze kama Movie (Royal Tour) ambayo itaitangaza Tanzania kwenye Mataifa ya Nje ili Tanzania iwekwe kwenye ramani ya Dunia, jambo hilo lilinigusa sana,tumpigie makofi Rais Samia”

“Kati ya Watu waliopata athari kutokana na Tanzania kutojulikana Mimi mmojawapo nimetembea Duniani kufundisha Watu wengi nakumbuka siku moja Tokyo nimefumdisha Watu zaidi ya Elfu 7 Wajapan, shida niliyokumbana nayo kila ukitaja Tanzania Watu wanasema tuoneshe kwenye ramani Tanzania iko wapi, ukisema Mlima Kilimanjaro wanasema upo Kenya, kuna vitu tunavikosa kwasababu Tanzania haijawa halisi sana kwenye ramani ya Dunia”

“Ni kazi ngumu sana kwa Rais ambaye ana majukumu mengi kujitolea yeye mwenyewe na kuanza kui-market Nchi yake , inagharimu muda, inagharimu sacrifice, inagharimu kuumia, hili jambo alilofanya Rais limekuwa zuri sana, tunatakiwa kumuuunga Mkono Rais”

“Madini, vivutio vyetu, amani yetu, vitafahamika huko nje na uchumi wetu utakua , Rais anatakiwa kutiwa moyo kwa silimia zote” ———Askofu Gwajima akiwa Kanisani Ufufuo na Uzima leo
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger