Hiki hapa Chanzo cha Shule ya Sekondari Gichameda kuungua moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Na John Walter -Manyara
Kufutia tukio la moto kuteketeza  ofisi ya walimu katika shule secondari ya Gichameda iliyopo  wilaya ya Babati mkoani Manyara,Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa limeeleza chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme katika jengo hilo.

Akizungumza na kituo hiki Kamishna msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Manyara [ACP] Gilbert Mvungi amesema mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia mwema kupitia namba ya 114 jeshi hilo lilifika eneo la tukio saa nane na dk 45 mchana.

Aidha ameongeza kuwa moto huo uliunguza ofisi ya walimu na vitabu mbalimbali ambavyo viliteketea, pamoja na ofisi ya fedha huku  ya makamu mkuu wa shule ambapo hata hivyo juhudi zilifanyika kuokoa nyaraka zilizpokuwemo katika ofisi hizo.

Sambamba na tukio hilo ACP Mvungi amewataka wakuu wa taasisi za umma na binafsi Mkoani Manyara  kuchuku a tahadhari ya moto kwa kuweka miundombinu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Gichameda Alex Joseph amesema alisikia kelele za watu wakiomba msaada ndipo akafika eneo la shule na kujionea tukio hilo la moto na kushirikiana na wananchi wengine wakaendelea kuokoa sehemu ya jengo hilo pamoja na nyaraka na kumbukumbu katika ofisi ya fedha.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ameeleza kuwa ofisi ya walimu na ofisi ya  makamu mkuu wa shule ndizo zilizo athirika na moto huo, licha ya juhudi mbalimbali za kuudhibiti kufanywa na wananchi usiku wa manane.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad