Maafisa 21 mbaroni kwa kutaka kufanya mapinduzi Sudan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Jeshi la Sudan limetoa taarifa likisema kwamba maafisa 21 na wanajeshi kadhaa wamekamatwa kuhusiana na jaribio la mapinduzi lililotokea leo asubuhi na msako unaendelea kuwakamata wengine waliobakia waliohusika na tukio hilo.



Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa jeshi ambaye ni mshauri wa masuala ya habari, Brigedia Jenerali Altahir Abu Haja, jeshi limeyadhibiti tena maeneo yote yaliyokuwa yamekamatwa wakati wa jaribio hilo.

Aidha serikali dhaifu ya mpito ya nchi hiyo imesema wanajeshi na raia waliohusishwa na jaribio hilo wanafungamanishwa na utawala ulioondolewa wa kiongozi wa muda mrefu, aliyeongoza kwa mkono wa chuma, Omar al-Bashir.

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amesema jaribio hilo ni njama za hivi karibuni za kuchochea mgogoro wa kitaifa, akigusia mgawanyiko mkubwa uliopo Sudan wakati ikielekea kwenye demokrasia.

Akihutubia kupitia Televisheni amesema waliopanga njama hiyo walifanya maandalizi ya kina ambayo yamejionesha kupitia mapungufu ya kiusalama yaliyoonekana mijini, kufungwa kwa barabara, bandari na uchochezi uliokuwa ukiendelezwa dhidi ya serikali ya kiraia.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad