.

9/11/2021

Hitimana Kocha Msaidizi Simba
KLABU ya Simba imemteua Thierry Hitimana (42) kuwa kocha msaidizi ikiwa ni hatua ya kuimarisha benchi lake la ufundi ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi kwenye michuano mbalimbali ambayo itashiriki.

 

Ofisa Mtendaji wa Simba Barbara Gonzalez amesema Gomez aliipa klabu ombi la kuongezewa msaidizi mwingine kwenye benchi la ufundi  na sifa za Hitimana zinakidhi.

 

Thierry  ni mmoja wa walimu wanaoheshimika Rwanda na aliwahi kuwa msaidizi wa Didier Gomez wakati Rayon Sports ikitwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

 

Mrwanda huyo ni msomi wa shahada ya Uzamili katika masuala ya Fedha aliopata nchini Ubelgiji ana leseni ya ukocha daraja A inayotolewa na CAF.

 

Simba ambayo inatetea ubingwa wa ligi msimu huu imejipanga pia kufanya vizuri kimataifa baada ya msimu uliopita kutupwa nje na Kaizer Chiefs ya Afrika kusini kwa mabao 4-3 katika hatua ya  robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Hitimana  amefundisha vilabu kadhaa vya ligi kuu Tanzania bara ikiwemo Mtibwa Sugar ya Morogoro, Biashara United ya Mkaonji Mara na Namungo Fc ya Lindi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger