Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Mbeya Kwanza yaanza vizuri ligi kuu, yaitandika Mtibwa Sugar
NYOTA  Willy Edgar Mwampamba mali ya Mbeya Kwanza leo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.
Ilikuwa ni dakika ya 49 nyota huyo alieza kufanya hivyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Kibaha wakati timu ya Mtibwa Sugar ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika 90 kwa kuwa Mtibwa Sugar walikwama kuweza kuweka mzani sawa na kuruhusu pointi tatu kusepa mazima na Wanambeya Kwanza.

Ni rekodi tamu kwa Mbeya Kwanza ya Mbeya ambayo imepanda daraja msimu huu kwa kuanza na kusepa na pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar.

Kocha Mkuu Joseph Omog leo alikuwa jukwaani akiwatazama vijana wake wakipoteza mchezo huo wa kwanza wa ligi na kipa wake Mshery kuwa wa kwanza kutunguliwa ndani ya msimu mpya.

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments