Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in amepiga marufuku ulaji wa nyama ya mbwa leo (Jumatatu), ofisi yake imesema, ikizungumzia utamaduni huo ambao umekuwa kero kwa jumuiya ya kimataifa.
Nyama hiyo imekuwa sehemu ya vyakula vya Korea Kusini, huku karibu mbwa milioni moja wakiaminika kuliwa kila mwaka, lakini matumizi yameporomoka katika miaka ya karibuni kutokana na watu kuanza kuchukulia wanyama hao kama marafiki badala ya mifugo.
Utamaduni huo sasa ni mwiko miongoni mwa kizazi kipya, huku shinikizo likiongezeka kutoka kwa wanaharakati wa haki za wanyama.