Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

MRISHO Gambo "Mama Yangu Alikuwa Muuza Uji Ilala, Baba Yangu Dalali wa Ndizi Sokoni"


Kwa historia Mimi Mrisho Gambo, Marehemu Mama yangu(ambaye ndiye alikuwa nguzo yangu) alikuwa Muuza uji Mchikichini Ilala(Mimi nikiwa msaidizi wake mkuu) na Baba yangu dalali wa ndizi sokoni Kariakoo. Sina ndugu yoyote kiongozi wala sina God Father. Nimeingia kwenye masuala ya Uongozi kwa kudra zake Mungu. Nina zungumza na wewe uliyekata tamaa Kwa kuwa toka umalize chuo hujapata kazi, au unafanya biashara lakini hujafanikiwa. Maisha ni Milima na mabonde, ukiona unakaribia kukata tamaa kwenye maisha jua mafanikio yako yapo karibu. Endelea kuwekeza matumaini yako kwa Mungu maana yeye huwa hawahi wala hachelewi bali ana wakati wake! Hata kwako inawezekana!

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments