Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Msanii AT kutoka Zanzibar Awashukia Cosota
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya na aliyejizolea umaarufu zaidi kwenye muziki wa mduara, @atmfalme amewashangaa COSOTA, chombo kinachosimamia Hakimiliki za wasanii,Baada ya hii leo Septemba 15 kutangaza rasmi suala la wasanii kulipwa kutokana na kazi zao huku msanii akipewa 70% na serikali ikichukua 30%.

AT amedai COSOTA wamejisahaulisha kuwa kuna pesa hadi leo hawajawalipa wasanii na pia kuwa COSOTA haina uwezo wa kukusanya Hela nje ya nchi ikizidiwa uwezo na COSOZA ya Zanzibar.

AT ameandika haya akijibu maoni ya msanii mwenzie @benjaminwamambojambo aliyedai hata hiyo 30% inayochukuliwa na serikali ni kubwa mno.

“ @benjaminwamambojambo unajuwa COSOTA wanajihisi km wanaakili sana leo wanakikao wanabahati sipo siku pata nafasi mapema ningeli watandika masuali hadi wangelijuta miaka 10 imepita hawajalipa sawanii wanajisahaulisha wanaanziashi ishu mpya hivi hawa ni wazima kweli? COSOTA enyewe uwezo wa kukusanya hela nje ya nchi hawana wanashinda hata na Cosoza ya Zanzibar 😂😂😂😂 wao ni kuongea mipango tu kila siku 😂😂😂😂😂 wasinipotezee time hawajawa yayari wasimamie BrCode kwanza watu walipwe Out side ya Tanzania”


 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments