Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Omog Atajwa Mtibwa Sugar
BAADA ya aliyetarajiwa kuwa Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thierry kutimkia Simba, inatajwa kuwa uongozi wa timu hiyo upo kwenye mazungumzo na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.

 

Omog aliwahi kuzinoa timu Azam FC na Simba. Hitimana aliondoka Mtibwa hivi karibuni wakati akiendelea kusimamia mazoezi ya timu ambayo iliweka kambi jijini Dar kujiandaa na michuano mbalimbali ya msimu ujao.

 

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema: “Unajua mwanzo tuliweka tangazo la kutafuta kocha mpya, zilikuja CV za makocha 70 hivyo uongozi ulikaa na kuchambua pia baadaye zikabaki tatu ambapo uongozi uliamua kumrudisha Hitimana.

 

“Baada ya kuondoka sasa viongozi pia wanafanya mchakato na jina la Omog ni moja kati ya CV ambazo zimetufikia, hivyo tusubiri kuona uongozi utaamua nini juu ya hilo.”

 Hawa Aboubakhari, Dar es Salaam

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments