.

9/03/2021

Samia aibua upya mradi wa Bandari ya Bagamoyo
 
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, mkoani Pwani ikiwa kutafanyika marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye mkataba ambavyo vinakwaza.

Aidha, amesema serikali inaondoa vipengele ambavyo awali vilikwamisha mradi huo kuendelea na kwamba ukikamilika utafungua fursa za kiuchumi, ikiwamo kuongeza wigo wa ajira kwa wakazi wa Bagamoyo na mikoa mingine.

Rais Samia aliyasema hayo jana katika eneo la Zinga, wilayani hapa alipozungumza na wananchi hao katika ziara maalum na kuwatoa hofu wakazi wa eneo hilo kuhusu fidia na kwamba mambo mazuri yanakuja kwa kuwa kila mtu atapata stahiki zake.

”Tunajua mradi ukiwa hapa wana Bagamoyo wote watapata ajira pale ni mradi mkubwa sana. Najua tuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana. Mradi ule utaleta mapato na utamaliza changamoto zote kama maeneo hayana umeme utaleta umeme,” alisema.

Pia aliwahakikishia wananchi hao kuwa miradi yote ambayo ilianza itamalizika na miradi mingine itaanzishwa, na kwamba bandari italeta maendeleo ikiwamo kufikisha huduma muhimu kwa wananchi ambazo ni pamoja na maji na umeme.


 
Kutekelezwa kwa mradi huo kutafungua maendeleo kwa wananchi na kutoa ajira kwa vijana wa Bagamoyo, lakini utafungua pia njia katika pande mbalimbali kwenye mji huo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, alimwomba Rais Samia kuwekewa taa Uwanja wa Ndege wa Mafia ili ndege kutua muda wote.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, aliishukuru serikali kwa mradi wa maji itakayotatua kero ya maji na kumtua mama ndoo.


Naye Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, alikumbushia ahadi ya Hayati Rais John Magufuli ya kupandisha hadhi Halmashauri ya Chalinze kuwa wilaya ili kusogeza huduma za jamii karibu na wananchi.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger