Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Simbachawene azungumzia video ya waliovua nguo ukumbini, taa kuzimwa


 Simbachawene amesema wameutambua ukumbi lilikotokea tukio la mwanamke na mwanaume kuvua nguo hadharani na baadhi ya watu wamekamatwa na wengine wanatafutwa.

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakiwa katika ukumbi huo huku mtu mmoja akitangaza kuwa wahusika ambao ni mwanamke na mwanaume watavua nguo jambo ambalo lilitekelezwa na wawili hao kisha taa zikazimkwa huku baadhi ya watu ukumbini hapo wakitumia simu kurekodi tukio hilo.

 “Vueni nguo kisha mtakutana katikati kitakachotokea mimi sijui,” amesikika akisema mshereheshaji wa shughuli hiyo huku wawili hao wakiwa watupu  wakisakata muziki na kusogeleana na kisha kukumbatiana.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 16, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari, Simbachawene amesema kwa sasa hawezi kueleza idadi ya waliokamatwa wala majina yao kwa kuwa upelelezi unaendelea.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments