Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Vijana Wawili Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Baada ya Kukutwa na Hatia ya Kumteka Mtoto na Kumuuwa
Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, imewahukumu watu wawili kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuteka mtoto wa miaka 12 na kuwataka wazazi wake wawape fedha kiasi cha milion 5 ili wamuachie mtoto ambaye walimuuwa na kumzika akiwa amekaa huku amefungwa mikono na kichwani.Tabibu Nyundo na Thobias Mtakiyicha, waliohukumiwa kunyongwa

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Tabibu Nyundo na Thobias Mtakiyicha wakazi wa Kijiji cha Gwanumpu wilaya ya Kakonko waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia kesi namba 18 ya mwaka 2021.

Imeelezwa kuwa mnamo Januari 27, 2021, washtakiwa walishirikiana kumteka mtoto huyo kisha kumtumia ujumbe wa simu jirani wa familia yake kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 5 ili wamuachie mtoto wao.

Source: EATV

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments