Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Yanga Bingwa Ngao ya Jamii, Yaichapa Simba 1-0
TIMU Yanga  ya leo Septemba 25, imefanikiwa , kuwanyanyasa watani wao wa jadi Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii,  baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliochezwa kwenye dimba la Mkapa Dar, Mchezo huo wa ambao unashiria kufungua kwa pazia la ligi kuu Tanzania Bara.

 

Goli pekee la Yanga limewekwa na Mshambuliaji Fiston Mayele aliyefunga dakika 12, ya mchezo, Yanga imefikia rekodi ya Simba ya kutwaa ngao ya Jamii kwa mara ya sita.

 

Kikosi cha Wananchi leo kilikuwa na wachezaji Khalid Aucho, Fiston Mayele na Yannic Bangala ambao wameonyesha kiwango bora dhidi ya Simba.

 

Kwenye mchezo huo Tadeo Lwanga alilimwa Kadi Nyekundu baada ya kumchezea rafu Feisal Salum.

 HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Post a Comment

0 Comments