Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

Korea Kaskazini yarejesha mawasiliano ya simu na Korea Kusini

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Korea Kaskazini (KCNA), Nchi hiyo imeamua kufungua laini zote za Mawasiliano ya Simu na Korea Kusini kuanzia leo, Oktoba 4

Ripoti zimesema uamuzi huo ulitangazwa baada ya ahadi iliyotolewa na Kiongozi Kim Jong-Un ikiwa kama juhudi za kutimiza matarajio na hamu ya Wananchi wote ambao wanataka kuona uhusiano kati ya Kaskazini na Kusini unarejeshwa


Uhusiano kati ya Nchi hizo mbili hauko vizuri tangu mkutano kati ya Korea Kaskazini na Marekani kutofikia makubaliano mapema Mwaka 2019.

 Downlaod App ya BLOG Hii Kutoka Google Play Kwa Kubonyeza HAPA>>>

Post a Comment

0 Comments