Mchoraji wa Katuni ya Mtume Muhammad, Lars Vilks Afariki kwa Ajali ya Gari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mchoraji wa vibonzo raia wa Sweden ambaye alichora mchoro wa Nabii Muhammad kwenye kiwiliwili cha mbwa amefariki Dunia katika ajali ya barabarani kulingana na vyombo vya habari.


Muhammad cartoonist Lars Vilk killed in car crash while under police protection | The Independent

Lars Vilks alikuwa akisafiri katika gari la kiraia la polisi ambalo liligongana na lori karibu na mji wa Markaryd kusini mwa Sweden.

Maafisa wawili wa polisi waliuawa na dereva wa lori alijeruhiwa.

Vilks, mwenye umri wa miaka 75, amekuwa akiishi chini ya ulinzi wa polisi waliomlinda baada ya kupata vitisho vya kuuawa kutokana na kibonzo hicho.


Kibonzo hicho, kilichochapishwa mwaka 2007, kiliwakera Waislamu wengi ambao waliuona uchoraji wa picha ya Nabii kama kukufuru.

Hii ilikuja mwaka mmoja baada ya gazeti la Denmark kuchapisha vibonzo vya Mtume Muhammad.

Polisi bado hawajafichua utambulisho wa wale waliouawa katika tukio hilo la Jumapili, lakini mwenzi wa Vilks amethibitisha kifo chake katika gazeti la Dagens Nyheter.


Taarifa ya polisi ilisema bado haijawa wazi jinsi mgongano wa magari hayo ulivyotokea, lakini awali hapakuwa na kitu chochote kilichoonyesha kuwa kuna mtu yeyote aliyehusika.

Kibonzo hicho kilisababisha hasira kubwa kutoka kwa umma na kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Fredrik Reinfeldt kukutana na mabalozi kutoka nchi 22 za Kiislamu kujaribu kutuliza hali.

Muda mfupi baadaye, kikundi cha al-Qaeda nchini Iraq kilitangaza kutoa $100,000 (£73,692) kama zawadi kwa yeyote atakayemuua.

Mnamo mwaka 2015, Vilks alishiriki mjadala kuhusu uhuru wa kujieleza ambao ulilengwa na shambulio la bunduki katika mji wa Copenhagen. Alisema huenda alikuwa mlengwa wa shambulio hilo, ambalo lilimuua muelekezaji mmoja wa filmu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad