Ticker

6/recent/ticker-posts

 .

50 Cent Afunguka Kuhusu Kipande Cha Risasi Kilichopo Katika Ulimi Wake "Daktari Aliogopa Kukitoa"Mara paap ndinga inakatiza mitaa ya Karibu kabisa na nyumba ya Bibi yake mida fulani hivi bila kuelewa hili wala lile Mchizi alikuwa nje Zikamiminika Risasi kama 9 na kumjeruhi sehemu mbali mbali ya mwili wake akiwa na miaka 25 tu .
.
Kwa mujibu wake Ni tukio ambalo hawezi kulisahau kabisa Sababu ingeondoa uhai wake lakini bahati nzuri alisalimika, Risasi zilipenya kwenye mikono, miguu, Kifua mpaka kwenye shavu lake la kushoto kiasi kwamba ilisababisha Matatizo makubwa kwake .
.
Huyu ni Rapa 50 Cent ambaye alisema kuwa Bado mpaka hii leo anaishi na kipande cha risasi ndani ya ulimi wake ambaco kimeathiri kuongea kwake na Rapa huyo alisema Daktari alihofia kutoa Risasi hiyo kwasababu ingeharibu ladha na kuketa madhara makubwa zaidi ( kwahiyo huu ni mwaka wa 21 Mchizi anaishi na Kipande cha Risasi )
.
Vile ambavyo mchizi anaimba na kuongea Ni sababh ya Kipande cha Risasi lakini pia 50 cent alisema kuwa hiyo ndio sauti inayofanya kazi, ile ambayo MUNGU aliacha aifanye mpaka sasa .
.
Curtis Jackson A.K.A 50 Cent Alilelewa katika kituo cha watoto Yatima akiwa na miaka 8 baada ya mama yake mzazi kufariki ambaye alikuwa akijihusisha na Uuzaji wa Dawa za kulevya, 50 aliingia mtaani na yeye kuendeleza kile alichokuwa akifanya Bi Mkubwa akiwa na miaka 12 .
.
50 Amekulia mtaani tu akiwa na ndoto siku moja atafanikisha na kufika kule ambako anahitaji kufika, kupitia kitabu cha "The 50th Law of Power" ambacho kimeandikwa kwa usaidizi wa Robert Greene imeandikwa kuwa 50 alikuwa Mchakalikaji ambaye hakuhitaji kabisa maisha yake yote kuishia mtaani kama Muuzaji wa Dawa za kulevya kwahiyo alibadilisha upepo wa utafutaji wake wa mkwanja .
.
Muziki ulikuja baadae mengi kupitia nyimbo zake kuna line zinaongelea lifestyle yake na kupitia wimbo wa Ghetto Quran umeeleza kuhusu Kenneth McGriff ambaye ndiyo alihusika kumlipa kijana Darry akamtwange Risasi .

Leo hii ni Muigizaji, mfanya biashara, Mwanamuziki na Producer pia -- .

 HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWA APP YA UDAKU SPECIAL, DOWNLOAD HAPA KUZISOMA HATA KAMA HUNA BUNDLE

 Udaku Special Blog

Post a Comment

0 Comments