Bastola ya Marekani yakamatwa Tanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga, limekamata Bastola aina ya Trurus ambayo imetengenezwa nchini Marekani, ikiwa na risasi 5 pamoja na magazine yake na iliyokuwa inamilikiwa bila kibali halali.


Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Safia Jongo wakati akitoa taarifa ya mwezi Oktoba, 2021 ambapo ameeleza pia wamegundua kiwanda cha kutengenezea bunduki za kienyeji aina ya Gobore baada ya msako mkali kuendeshwa na Jeshi la Polisi.



"Tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja mwanaume ambaye alikuwa na mtambo wa kutengeneza hayo magobore na alikuwa na magobore 11, pamoja na vifaa vya kutengeneza silaha, kama Trigger, Cockinhandle ambayo inatumika katika silaha hizo", alisema ACP Jongo.



Aidha ACP Jongo aliongeza kuwa, "Operesheni ilipangwa kimkakati tumekuwa na matumizi mabaya ya silaha hizo aina ya gobore katika misitu yetu, hivyo ikatulazimu kupanga mikakati kujua ni wapi yanapotoka".



Hata hivyo ameongeza kuwa kwenye operesheni hiyo wamekamata kilo 372 za mirungi pamoja na pikipiki 12 ambazo zilikua zikisafirisha mirungi na wahamiaji haramu.

 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad