Bwana harusi kizimbani akidaiwa kutaka kumuoa mwanafunzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Mkazi wa kitongoji cha Ujerumani, Baraka Kulwa aliyetaka kumuoa mwanafunzi wa darasa la sita mwenye miaka 14 pamoja na mama mzazi wa binti huyo, wamefikishwa  katika  mahakama ya hakimu mkazi wilaya kwa tuhuma za kumuoa na kumuozesha mwanafunzi huyo.


Wakisomewa maelezo ya awali mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Serikali,  Damas Chonya mbele ya hakimu mkazi, Jullius Mhanusi, imedaiwa walitenda kosa hilo Novembea 10, 2021.



Amesema  walikamatwa na polisi wakiwa kwenye harusi ya kimila baada ya polisi  kupewa taarifa za siri na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kuwa kuna  mwanafunzi anaozeshwa na ndipo walianza ufuatiliaji na kufanikisha kuwakamata wakiwa kwenye sherehe.



Chonya aliwataja waliokamatwa kuwa ni bwana harusi, Baraka Kulwa (26), Rashid Saidi (40), mama wa binti huyo, Stumai Sakenge (35), mpambe wa bwana harusi, Sadam Shaban (18) pamoja na mama wa bwana harusi, Sandu Sandu Maduhu(55) wote wakazi wa kitongoji cha Ujerumani.



Baada ya kusomewa mashtaka wote walikana kosa lao na mwendesha mashtaka amesema upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwamba kesi hiyo itaendelea Novemba 25, 2021 na  washtakiwa walirudishwa rumande kutokana na  kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad