Sindano Mbadala ARVs Yaidhinishwa, Wenye VVU Wanachomwa Mara 6 kwa Mwaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



TAASISI ya Usimamizi wa Dawa nchini Uingereza (NHS) pamoja na mashirika mengine ya msaada imeidhinisha matibabu ya sindano mpya yenye ufanisi wa muda merefu kwa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sindano hiyo husitisha makali ya VVU sawa na dawa za kawaida za kufubaza makali ya VVU – antiretroviral maarufu kama ARVs

Inakadiriwa kuwa watu 13,000 nchini Uingereza wanaweza kuamua kudungwa sindano hiyo badala ya kumeza vidonge hivyo kila siku.

Dawa hiyo ya sindano inayotengenezwa na ViiV Healthcare inafahamika kama Cabotegravir au Vocabria wakati inayoitwa Rekambys inatengenezwa na kampuni ya Janssen.


Sindano hiyo hutolewa mara mbili kwa muda tofautii kila baada ya miezi miwili.

Tiba hiyo ni bora tu kwa wale ambao wamefanikiwa kufikia viwango vya kutogundulika kwa virusi katika damu yao wakati wanapomeza vidonge.




Wataalamu wanasema tiba hii ya sindano inaweza kuwa rahisi na kutumiwa na wengi.

Profesa Chloe Orkin, ambaye ni mtaalam wa VVU kutoka Chuo kikuu cha Queen Mary cha London, amesema itawapunguzia mzigo watu wenye VVU ambao wamekuwa wakilazimika kumeza vidonge kila siku na badala yake kuwapatia tiba mara sita tu kwa mwaka.

Dk. Sanjay Bhagani, rais taasisi ya tiba ya Ukimwi – European Aids Clinical Society, amesema “Hili limepokelewa vyema kabisa.

“Bado unyanyapaa umebaki kuwa changamoto kwa jamii ya watu wenye VVU, na kumeza tembe kila siku ni jambo linaloweza kuwa gumu miongoni mwa baadhi ya watu. Hii inatoa tiba mbadala ya sindano kwa wengi.




“Takwimu na tafiti zinazoshauri tiba hii ni imara na uzoefu halisi wa dunia unaonyesha kwamba wagonjwa wanaoanza kwa tiba za sindano hupendelea kuendelea nazo.”


Alex Sparrowhawk, kutoka Manchester, anafanya kazi katika shirika la msaada linalowasaidia wanaoishi na VVU linaloitwa Terrence Higgins Trust.

Alibainika kuwa na VVU miaka 12 iliyopita na amekuwa akipokea dawa za ART tangu wakati huo. Anasema kuwa na chaguo tofauti la tiba ni jambo la kufurahisha.

“Habari hii mpya ni kitu ambacho watu wengi wamekuwa wakikisubiri.

“Wazo la kudungwa sindano mara sita kwa mwaka badala ya kumeza vidonge kila siku bila shaka linafurahisha. Kukumbuka kumeza vidonge kila siku ni jambo linalohitaji umakini mkubwa,” amesema.

Anaamini wale wanaohitaji zaidi tiba mpya, kama vile wake wanaonyanyapaliwa zaidi, wanafaa kupewa kipaumbele kupewa tiba ya sindano.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad