Tuendelee na vioja vya @ericomondi , Jamaa anataka Ngoma za wasanii wa kenya Zipigwe zaidi kwenye Redio kuliko ngoma za wasanii kutoka nje ya Kenya.
Pia Anadai kwamba DJs wa Clubs mbalimbali ndani ya kenya wapige ngoma nyingi za wakenya kuliko za Wasanii kutoka nje ya Kenya.
Jamaa anajichanganya zaidi na kuonekana kama anapambania kitu ambacho haelewi madhara yake mbeleni hasa pale anaposema kwamba Kufikia mwakani anataka wasanii wa kenya wawe wa kimataifa zaidi, wapige show USA nakadharika
Huyu jamaa kweli hajielewi, je kwa mfano kila nchi ichukue uamuzi kama wake, Kwamba kila nchi iazimie kupiga ngoma zao tu, je hao wasanii wa kenya watapenyaje katika soko la kimataifa? maana kila nchi itakuwa inapiga nyimbo za wasanii wake tu...so hakuna msanii yoyote atakayetoboa Kimataifa, wote wataishia kuwa wasanii wa ndani ya nchi tu.
Eric Omondi pamoja na wafuasi wake wanatakiwa kujiuliza kwanza, Je kwanini ngoma za kenya hazipigwi sana Redioni na Club? Wakishapata majibu ndio warudi na Mbinu mpya, Inawezekana Ngoma za Kenya ni mbaya, hazishawishi Media na Djs Kuzitumia katika Shughuli zao.
Ngoma ikiwa kali itapigwa tu, eric omondi aache ushamba, mbona Tz Tunapiga sana ngoma za WillyPaul, SautSol, ile ngoma ya MEJJA "UTAWEZANA" ulikuwa wimbo wa taifa huku, kila kona ulipigwa, lakini hakuna mbongo aliyekasirika.
@coymzungu nadhani unaona harakati za Rafiki yako @Ericomondi, tutashangaa sana Siku ukimleta kwenye events za Cheka tu