6/09/2022

Nimemuambia Wife Awe Anasuka Style hii ya Nywele ili ku-Save Cost, Kaishia Kunisunya na Kunibinulia Midomo

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Kwema ndugu zangu watanganyika? Kutokana na mimi kupitia changamoto za kifedha kwa sasa, nilimuomba Wife tupunguze gharama za uendeshaji wa maisha yetu kwa kujibana sana, pendekezo langu la kwanza nilipendekeza Wife anyoe nywele zake alizosuka, akajitetea kwamba nywele zake katumia karibia miaka 10 kuzifikisha hapo zilipofikia hivyo hatoweza kuzinyoa na akaongezea kuwa akinyoa yeye huwa ana kichwa kibaya hivyo hatokua comfortable.

Basi mimi nikajaribu kupitia kwenye baadhi ya pages za wadada wenye saloon huko Instagram nikaja na pendekezo moja kuwa Wife awe anasuka style fulani hivi ya nywele ambayo ni affordable kwani ni elfu 5 tu ila mwenzangu nilipomshirikisha hivyo akaishia kunisunya na kunibinulia midomo kuwa hayuko tayari.

Mpaka sasa kaninunia ila mimi msimamo wangu uko pale pale sitotoa zaidi ya elfu 5 ya kusukia.

Asanteni

By Mdau

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger